1 Corinthians 15:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini vitu vyote vitakapowekwa chini ya utawala wa Kristo, ndipo naye Mwana atakapojiweka chini ya Mungu, aliyeweka vyote chini ya utawala wake; ili Mungu atawale juu ya vyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atakapokuwa amekwisha kuyafanya haya, ndipo Mwana mwenyewe atatiishwa chini yake yeye aliyetiisha vitu vyote, ili Mungu awe yote katika yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya kuweka kila kitu chini ya Kristo, ndipo yeye mwenyewe, kama Mwana, atawekwa chini ya Mungu. Katika namna hii Mungu atakuwa mtawala mkuu juu ya kila kitu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini vitu vyote vitakapowekwa chini ya Utawala wa Kristo, ndipo naye Mwana atakapojiweka chini ya Mungu, aliyeweka vyote chini ya Utawala wake; ili Mungu atawale juu ya vyote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini vitu vyote vitakapowekwa chini ya utawala wa Kristo, ndipo naye Mwana atakapojiweka chini ya Mungu, aliyeweka vyote chini ya utawala wake; ili Mungu atawale juu ya vyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atakapokuwa amekwisha kutiisha vitu vyote chini ya Mwana, ndipo Mwana mwenyewe atatiishwa chini yake yeye aliyetiisha vitu vyote, ili Mungu awe yote katika yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atakapokuwa amekwisha kuyafanya haya, ndipo Mwana mwenyewe atatiishwa chini yake yeye aliyetiisha vitu vyote, ili Mungu awe yote katika yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini vitu vyote vitakapowekwa chini ya utawala wa Kristo, ndipo naye Mwana atakapojiweka chini ya Mungu, aliyeweka vyote chini ya utawala wake; ili Mungu atawale juu ya vyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hapo, yote yatakapokuwa yamekwisha kuwekwa chini yake, ndipo, naye Mwana mwenyewe atajiweka chini yake yule aliyeyaweka yote chini yake. Maana yote yawe yake Mungu po pote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wakati vitu vyote vitakapokuwa vimewekwa chini ya mamlaka ya Mwana, halafu yeye mwenyewe atajiweka chini ya mamlaka ya Mungu aliyemupa mamlaka juu ya vitu vyote, kusudi Mungu apate kutawala juu ya vyote kabisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe nae atatiishwa chini yake aliyemtiishia vitu vyote, illi Mungu awe yote katika yote.