1 Corinthians 15:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama kusudi langu lingalikuwa la kibinadamu tu, kule kupigana kwangu na wanyama wakali hapa Efeso kungalinifaa kitu gani? Kama wafu hawafufuki, basi, “Tule na tunywe, maana kesho tutakufa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama kwa sababu za kibinadamu tu nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, ningekuwa nimepata faida gani? Kama wafu hawafufuliwi, “Tuleni na kunywa, kwa kuwa kesho tutakufa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Niliwapiga wanyama wa porini kule Efeso. Ikiwa nilifanya hivyo kwa sababu za kibinadamu tu, sijapata kitu. Ikiwa hatufufuliwi kutoka kwa wafu, “basi tule na tunywe, kwa sababu tutakufa kesho.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama kusudi langu lingalikuwa la kibinadamu tu, kule kupigana kwangu na wanyama wakali hapa Efeso kungalinifaa kitu gani? Kama wafu hawafufuki, basi, “Tule na tunywe, maana kesho tutakufa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama kusudi langu lingalikuwa la kibinadamu tu, kule kupigana kwangu na wanyama wakali hapa Efeso kungalinifaa kitu gani? Kama wafu hawafufuki, basi, “Tule na tunywe, maana kesho tutakufa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama kwa tumaini la kibinadamu tu nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, ningekuwa nimepata faida gani kwa jambo hilo? Kama wafu hawafufuliwi, “Sisi na tule na kunywa, kwa kuwa kesho tutakufa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama kwa sababu za kibinadamu tu nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, ningekuwa nimepata faida gani? Kama wafu hawafufuliwi, “Tuleni na kunywa, kwa kuwa kesho tutakufa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nilipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama kusudi langu lingalikuwa la kibinadamu tu, kule kupigana kwangu na wanyama wakali hapa Efeso kungalinifaa kitu gani? Kama wafu hawafufuki, basi, “Tule na tunywe, maana kesho tutakufa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama nimeshindana na nyama wakali kimtu tu huko Efeso, vingenifaliaje? Wafu wasipofufuka, basi: Na tule, na tunywe! Kwani kesho tutakufa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa ni kwa nia ya kimutu, nimepigana na nyama wakali wa pori katika Efeso, jambo lile limenifalia nini? Kama wafu hawafufuki, basi: “Tukule na tukunywe, kwa maana kesho tutakufa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na nyama wakali kule Efeso, nina faida gani wasipofufuka wafu? Tule, tukanywe, maana kesho tutakufa.