1 Corinthians 15:35 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mtu anaweza kuuliza: “Wafu watafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mtu mmoja anaweza kuuliza, “Waliokufa wanafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mtu anaweza kuuliza: “Wafu watafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani wakati watakapokuja tena?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mtu anaweza kuuliza: “Wafu watafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini labda mtu atasema, Wafu wafufuliwaje? Nao huja kwa mwili gani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mtu anaweza kuuliza: “Wafu watafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini labda yuko atakayeuliza: Wafu watafufukaje? Nao watakuja wenye miili gani?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini labda kuko mutu anayeweza kuuliza: “Namna gani wafu watafufuka? Nao watakuwa na mwili wa namna gani wakati ule watakaporudia?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Labda mtu atasema, Wafufukaje wafu? Na kwa mwili gani waja?