1 Corinthians 15:50 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ndugu, nasema hivi: Kile kilichofanywa kwa mwili na damu hakiwezi kuushiriki ufalme wa Mungu; na chenye kuharibika hakiwezi kuwa na hali ya kutoharibika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndugu zangu nisemalo ni hili: mwili na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninawaambia hili ndugu zangu: Miili yetu na nyama na damu haiwezi kuwa na nafasi katika ufalme wa Mungu. Kitu kitakachoharibika hakiwezi kuwa na sehemu katika kitu kisichoharibika kamwe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, ndugu, nasema hivi: kile kilichofanywa kwa mwili na damu hakiwezi kuushiriki Ufalme wa Mungu; na chenye kuharibika hakiwezi kuwa na hali ya kutoharibika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ndugu, nasema hivi: kile kilichofanywa kwa mwili na damu hakiwezi kuushiriki ufalme wa Mungu; na chenye kuharibika hakiwezi kuwa na hali ya kutoharibika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndugu zangu nisemalo ni hili: nyama na damu haviwezi kuurithi Ufalme wa Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndugu zangu nisemalo ni hili: nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mwenyezi Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutoharibika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ndugu, nasema hivi: Kile kilichofanywa kwa mwili na damu hakiwezi kuushiriki ufalme wa Mungu; na chenye kuharibika hakiwezi kuwa na hali ya kutoharibika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu, hili nalisema waziwazi: Yenye nyama na damu haiwezi kuurithi ufalme wa Mungu, wala yenye kuoza haitairithi isiyooza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu zangu, muangalie, jambo ninalotaka kusema ni hili: kile kilichoumbwa kwa nyama na damu hakiwezi kupata urizi katika Ufalme wa Mungu katika hali ile, wala hakuna chenye hali ya kuharibika kinachoweza kuwa na hali ya kutoharibika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nisemayo ni haya, ndugu, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharihika.