1 Corinthians 15:58 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, ndugu zangu wapendwa, simameni imara. Msitikisike. Mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana Isa, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana Isa si bure.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo, kaka na dada zangu, simameni imara. Msiruhusu kitu chohote kiwabadilishe. Jitoeni nafsi zenu kikamilifu kwa kazi yenu katika Bwana. Mnajua ya kuwa chochote mnachofanya kwa ajili ya Bwana hakitapotea bure bila manufaa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu si bure katika Bwana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana Isa, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana Isa si bure.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo, ndugu zangu wapendwa, mjishupaze, msitukutike! Jikazeni kuendelea kazini mwa Bwana po pote, kwa kuwa mmejua, ya kama masumbuko yenu, mnayoyaona kwa ajili ya Bwana, siyo ya bure!*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wandugu zangu wapenzi, musimame imara bila kutikisika. Muendelee kumutumikia Bwana siku zote, mukijua kwamba masumbuko munayopata kwa ajili ya Bwana hayatapita bure.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.