1 Corinthians 16:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja na ndugu wengine, lakini hapendelei kabisa kuja sasa ila atakuja mara itakapowezekana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi kwa habari za ndugu yetu Apolo, nimemsihi kwa bidii aje kwenu pamoja na hao ndugu. Ingawa alikuwa hapendi kabisa kuja sasa, lakini atakuja apatapo nafasi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kwa habari za Apolo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja na hao ndugu; ambaye si mapenzi yake kwenda sasa; lakini atakuja atakapopata nafasi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na sasa kuhusu Apolo: Ninamsihi sana aje na ndugu wengine kuwatembelea ninyi huko Korintho. Hajataka kuja sasa, lakini atakuja kwenu atakapopata nafasi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja na ndugu wengine, lakini hapendelei kabisa kuja sasa ila atakuja mara itakapowezekana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja na ndugu wengine, lakini hapendelei kabisa kuja sasa ila atakuja mara itakapowezekana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi kwa habari za ndugu yetu Apolo, nimemsihi kwa bidii aje kwenu pamoja na hao ndugu. Ingawa alikuwa hapendi kuja sasa, lakini atakuja apatapo nafasi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi kwa habari za ndugu yetu Apolo, nimemsihi kwa bidii aje kwenu pamoja na hao ndugu. Ingawa alikuwa hapendi kabisa kuja sasa, lakini atakuja apatapo nafasi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kuhusu Apolo, ndugu yetu, nilimsihi sana aje kwenu pamoja na hao ndugu; ambaye si mapenzi yake kwenda sasa; lakini atakuja atakapopata nafasi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja na ndugu wengine, lakini hapendelei kabisa kuja sasa ila atakuja mara itakapowezekana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwa ajili ya ndugu yetu Apolo mjue, ya kuwa nimemhimiza mara kwa mara, aje kwenu pamoja na hao ndugu; lakini hakutaka kabisa kwenda sasa. Lakini atakuja, patakapomfalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kwa habari za Apolo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja na hao ndugu; ambaye si mapenzi yake kwenda sasa; lakini atakuja atakapopata nafasi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa ngambo ya ndugu yetu Apolo, nimemusihi sana akuje kwenu pamoja na wandugu wengine, lakini hakutaka kabisa kwenda sasa; atakwenda kwa wakati utakaomupendeza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini kwa khabari za Apollo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja nao ndugu, nae hakupenda kabisa kwenda sasa; lakini atakwenda sitakupopata nafasi.