1 Corinthians 16:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula na Priska pamoja na watu wote wa Mungu walio nyumbani mwao wanawasalimuni sana katika kuungana na Bwana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makundi ya waumini wa jimbo la Asia wanawasalimu. Akila na Prisila pamoja na kundi la waumini walioko nyumbani mwao wanawasalimu sana katika Bwana Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Makanisa ya Asia yanawasalimu. Akila na Priska wanawasalimu katika Bwana. Na kanisa linalokutana nyumbani mwao linawasalimu pia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula na Priskila pamoja na watu wote wa Mungu walio nyumbani mwao wanawasalimuni sana katika Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula na Priska pamoja na watu wote wa Mungu walio nyumbani mwao wanawasalimuni sana katika kuungana na Bwana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makanisa ya Asia yanawasalimu. Akila na Prisila, pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao wanawasalimu katika Bwana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makundi ya waumini ya Asia yanawasalimu. Akila na Prisila, pamoja na kundi la waumini lililoko nyumbani kwao, wanawasalimu sana katika Bwana Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula na Priska pamoja na watu wote wa Mungu walio nyumbani mwao wanawasalimuni sana katika kuungana na Bwana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wateule wote walioko Asia wanawasalimu. Akila na Puriskila pamoja nao wote wanaokusanyika nyumbani mwao wanawasalimu sana, kwa kuwa m wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makanisa ya jimbo la Azia yanawasalimia. Akila na Prisila pamoja na kanisa linalokusanyika ndani ya nyumba yao wanawasalimia sana katika Bwana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Makanisa ya Asia wawasalimu. Akula na Priskilla wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililo ndani ya nyumba yao.