1 Corinthians 16:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo nitakapowasili, nitawapa wale mtakaowachagua barua za kuwatambulisha, ili kuwatuma wapeleke zawadi zenu huko Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nitakapofika, nitatuma baadhi ya watu wapeleke sadaka yenu Yerusalemu. Hawa watakuwa wale ambao ninyi mtakubali kuwa waende. Nitawatuma na barua ya utambulisho.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo nitakapowasili, nitawapa wale mtakaowachagua barua za kuwatambulisha, ili kuwatuma wapeleke sadaka zenu huko Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo nitakapowasili, nitawapa wale mtakaowachagua barua za kuwatambulisha, ili kuwatuma wapeleke zawadi zenu huko Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nami nitakapofika nitawatuma kwa barua wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ndipo nifike, wale, mtakaowachagua ninyi, nitawatuma na barua, wavipeleke vipaji vyenu Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nami nitakapofika, nitatuma watu mutakaochagua, pamoja na barua kwa kupeleka zawadi yenu Yerusalema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nami nitakapofika nitawatuma wale mtakaowachagua kwa nyaraka, wachukue ihsani yenu hatta Yerusalemi.