1 Corinthians 16:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huenda nitakaa nanyi kwa muda, au hata kukaa nanyi kipindi chote cha baridi, ili mweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendapo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Labda nitakaa kwenu; naam, labda wakati wote wa baridi, mpate kunisafirisha ko kote nitakakokwenda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pengine nitakaa kwenu kwa muda. Pengine nitakaa kwenu majira yote ya baridi. Hivyo mtaweza kunisaidia katika safari yangu, kila ninapokwenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huenda nitakaa nanyi kwa muda, au hata kukaa nanyi kipindi chote cha baridi, ili mweze kunisaidia katika safari zangu, po pote niendapo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huenda nitakaa nanyi kwa muda, au hata kukaa nanyi kipindi chote cha baridi, ili mweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendapo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Labda nitakaa kwenu; naam, labda wakati wote wa baridi, mpate kunisafirisha kokote nitakakokwenda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini kwenu, kama vinapatikana, nitakaa, labda nitamaliza kwenu siku za kipupwe, ninyi mpate kunisindikiza huko nitakakokwenda
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Labda nitakaa kwenu; naam, labda wakati wote wa baridi, mpate kunisafirisha ko kote nitakakokwenda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Labda nitabakia pamoja nanyi muda kidogo, au tena wakati wote wa mvua kali; kusudi muweze kunisaidia kuendelea pahali popote nitakapokwenda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Labda nitakaa kwenu; naam, labda nitashinda kwenu wakati wa baridi, mpate kunisafirisha wakati uwao wote nitakapokwenda.