1 Corinthians 16:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana sitaki niwaone sasa na kupita tu; natarajia kuwa nanyi kwa muda wa kutosha, kama Bwana Isa akipenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraji kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sitaki kuja kuwaona sasa, kwa sababu nitaweza tu kukaa nanyi kwa muda mfupi, kabla haijanilazimu kwenda mahali pengine. Ninategemea kukaa pamoja nanyi kwa muda mrefu, ikiwa Bwana ataruhusu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana sitaki niwaone sasa na kupita tu, natarajia kuwa nanyi kwa muda wa kutosha, kama Bwana akipenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana sitaki niwaone sasa na kupita tu; natarajia kuwa nanyi kwa muda wa kutosha, kama Bwana Isa akipenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu natarajia kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani sasa sitaki kuonana nanyi kwa kupita tu; kwani nangojea, nikae kwenu kitambo cha siku, Bwana akipenda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraji kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana sitaki kuonana nanyi kwa kupita tu. Ninatumaini kukaa pamoja nanyi siku chache Bwana akitaka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana sitaki kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraja kukaa kwenu mda wa kitambo, Bwana akinijalia.