1 Corinthians 2:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunafundisha hekima kwa watu ambao macho yao yamefunguliwa ili waione hekima ya siri ya Mungu. Si hekima ya watawala wa ulimwengu huu wanaobatilika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Tena yako ya werevu wa kweli; tunawaambia wale wenye kuyatimiza yote. Lakini nayo siyo ya werevu wa ulimwengu huu, wala wa wakuu wa ulimwengu huu walio wenye kufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingawa vile, mimi ninatangaza mambo ya hekima kwa watu waliokomaa kiroho. Lakini mambo haya si ya hekima ya kidunia, wala ya watawala wa dunia hii watakaoangamizwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Illakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; nayo si hekima ya dunia hii, wala yao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilishwa;