1 Corinthians 2:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hekima tunayotumia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichika, ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufu wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuumbwa, kwa ajili ya utukufu wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunaisema hekima ya Mungu katika namna ambayo baadhi wanaweza kuiona na wengine hawawezi. Ni hekima iliyofichwa mpaka wakati huu na Mungu aliipanga hekima hii kabla ya kuumba ulimwengu, kwa ajili ya utukufu wetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hekima tunayotumia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichika, ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufu wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hekima tunayotumia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichika, ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufu wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika kwa wanadamu, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hekima tunayotumia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichika, ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufu wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ila yaliyo ya werevu wa Mungu ulio wa kweli ndiyo, tunayoyasema, nayo yalikuwa hayajatokea bado, maana yalikuwa yamefichwa; huko kale, ulimwengu ulipokuwa haujawa bado, Mungu aliyachagua yayo hayo, yatokee sasa kututukuza sisi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninatangaza hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichwa kwa watu, na iliyopangwa na Mungu mbele ya kuumbwa kwa dunia kwa ajili ya utukufu wetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali twanena hekima ya Mungu katika fumbo, ile iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu asili, kwa utukufu wetu;