1 Corinthians 2:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana wangaliielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati hizi aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangeelewa, hawangemsulubisha Bwana wa utukufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakuna mtawala yeyote wa ulimwengu huu aliyeielewa hekima hii. Ikiwa wangeielewa, wasingemwua Bwana wetu mkuu na mwenye utukufu mwingi msalabani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana wangalielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana wangaliielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati zetu aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangelielewa, wasingemsulibisha Bwana wa utukufu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati hizi aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangelielewa, wasingemsulubisha Bwana wa utukufu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana wangaliielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwao wanaoutawala ulimwengu huu hakuna aliyeyatambua. Maana kama wangaliyatambua, wasingalimwamba msalabani Bwana aliye mwenye utukufu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakuna hata mutawala mumoja kati ya watawala wa dunia hii aliyeelewa hekima ile. Kama wangeielewa wasingemutundika Bwana wa utukufu juu ya musalaba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ambayo wenye kutawala dunia hii hawakuijua hatta mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;