1 Corinthians 2:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona, wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ni kama ilivyoandikwa: “Hakuna jicho limepata kuona, wala sikio limepata kusikia, wala hayakuingia moyoni mwa mwanadamu yeyote, mambo ambayo Mungu amewaandalia wale wanaompenda”:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini kama Maandiko yanavyosema, “Hakuna aliyewahi kuona, hakuna aliyewahi kusikia, hakuna aliyewahi kufikiri kuhusu kile ambacho Mungu amewaandalia wanaompenda.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona, wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ni kama ilivyoandikwa: “Lile jambo ambalo jicho halijapata kuona, sikio halijapata kusikia, wala halikuingia moyoni, lile ambalo Mungu aliwaandalia wale wampendao”:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ni kama ilivyoandikwa: “Hakuna jicho limepata kuona, wala sikio limepata kusikia, wala hayakuingia moyoni wowote, yale Mungu amewaandalia wale wampendao”:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona, wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ila ilikuwa, kama ilivyoandikwa: Jicho lisiyoyaona, sikio lisiyoyasikia, moyo wa mtu usiyoweza kuyatia mwake, ndiyo, Mungu aliyowaandalia wale wampendao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ni kama vile Maandiko Matakatifu yanavyosema: “Mambo yale ambayo hakuna mutu aliyepata kuyaona wala kuyasikia, mambo yale ambayo hakuna mutu aliyepata kufikiri juu yake, ndiyo yale Mungu aliyowatayarishia wale wanaomupenda.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, Wala hayakuingia katika moyo wa kibinadamu, Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.