1 Corinthians 3:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msijidanganye! Mtu yeyote miongoni mwenu akijidhania mwenye hekima mtindo wa kidunia, heri awe mjinga kusudi apate kuwa na hekima ya kweli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msijidanganye. Kama mtu yeyote miongoni mwenu akidhani kuwa ana hekima kwa viwango vya dunia hii, inampasa awe mjinga ili apate kuwa na hekima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Msijidanganye. Yeyote anayejiona kuwa ana hekima kwa viwango vya ulimwengu huu, basi na awe mpumbavu. Hiyo ndiyo njia pekee itakayomfanya kuwa na hekima.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Msijidanganye! Mtu yeyote miongoni mwenu akijidhania mwenye hekima mtindo wa kidunia, heri awe mjinga kusudi apate kuwa na hekima ya kweli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msijidanganye! Mtu yeyote miongoni mwenu akijidhania mwenye hekima mtindo wa kidunia, heri awe mjinga kusudi apate kuwa na hekima ya kweli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msijidanganye. Kama mtu ye yote miongoni mwenu akidhani kuwa ana hekima kwa viwango vya dunia hii, inampasa awe mjinga ili apate kuwa na hekima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msijidanganye. Kama mtu yeyote miongoni mwenu akidhani kuwa ana hekima kwa viwango vya dunia hii, inampasa awe mjinga ili apate kuwa na hekima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msijidanganye! Mtu yeyote miongoni mwenu akijidhania mwenye hekima mtindo wa kidunia, heri awe mjinga kusudi apate kuwa na hekima ya kweli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu asijidanganye! Ikiwa mtu wa kwenu anajiwazia kuwa mwenye werevu wa kweli katika ulimwengu huu, sharti apumbae, apate kuwa mwerevu wa kweli!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote asijidanganye mwenyewe. Kama mutu fulani kati yenu akijizania kuwa mwenye hekima ya kidunia, ajifanye kama mupumbafu kusudi apate kuwa na hekima ya kweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu asijidanganye nafsi yake: kama mtu akijiona kuwa mweuye hekima kati yeuu katika dunia hii, na awe mpumbavu, apate kuwa mwenye hekima.