1 Corinthians 4:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika kuungana na Kristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata kama mnao walimu elfu kumi katika Al-Masihi, lakini hamna baba wengi. Mimi nilikuwa baba yenu katika Al-Masihi Isa kwa kuwaletea Injili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnaweza kuwa na walimu elfu kumi katika Kristo, lakini hamna baba wengi. Kupitia Habari Njema mimi nilifanyika baba kwenu katika Kristo Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika maisha ya Kikristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika kuungana na Kristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata kama mnao walimu 10,000 katika Kristo, lakini hamna baba wengi. Mimi nilikuwa baba yenu katika Kristo Yesu kwa kuwaletea Injili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata kama mnao walimu 10,000 katika Al-Masihi, lakini hamna baba wengi. Mimi nilikuwa baba yenu katika Al-Masihi Isa kwa kuwaletea Injili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu elfu kumi katika Kristo, lakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika kuungana na Kristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ingawa mnao wafunzi maelfu katika Kristo, lakini hamnao baba wengi. Kwani mimi ndiye niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa kuwapigia hiyo mbiu njema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi kuelekea maisha yenu na Kristo, hata mukiwa na walezi maelfu muko tu na baba mumoja. Kwa maana kuelekea maisha yenu na Yesu Kristo ni mimi niliyewazaa kwa njia ya kuwatangazia Habari Njema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana mimi ndiye aliyewazaa katika Kristo Yesu kwa Injili.