1 Corinthians 4:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndiyo maana nimemtuma Timotheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika kuungana na Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuungana na Kristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu hii ninamtuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana Isa. Yeye atawakumbusha kuhusu njia za maisha yangu katika Al-Masihi Isa, ambayo yanakubaliana na mafundisho yangu ninayofundisha katika kila kundi la waumini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo sababu ninamtuma Timotheo kwenu. Ni mwanangu katika Bwana. Ninampenda na ni mwaminifu. Atawasaidia ili mkumbuke namna ninavyoishi kama mfuasi wa Kristo Yesu, kama ninavyofundisha katika kila kanisa kila mahali ninakokuwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndiyo maana nimemtuma Timetheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuishi maisha ya Kikristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndiyo maana nimemtuma Timotheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika kuungana na Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuungana na Kristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu hii ninamtuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana. Yeye atawakumbusha kuhusu maisha yangu katika Kristo ambayo yanakubaliana na mafundisho yangu ninayofundisha kila mahali kwenye kila kanisa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu hii ninamtuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana Isa. Yeye atawakumbusha kuhusu njia za maisha yangu katika Al-Masihi Isa, ambayo yanakubaliana na mafundisho yangu ninayofundisha katika kila kanisa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndiyo maana nimemtuma Timotheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika kuungana na Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuungana na Kristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hii nimemtuma Timoteo kwenu, huyu ni mtoto wangu mpendwa na mwelekevu katika Bwana. Yeye atawakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama ninavyowafundisha wateule wote po pote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni kwa sababu hii ninawatumia ninyi Timoteo. Yeye ni mwana wangu mupendwa na mwaminifu mbele ya Bwana. Atawakumbusha kanuni ninazofuata katika maisha yangu na Yesu Kristo, nami ninazofundisha fasi zote katika makanisa yote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa hiyo nalimtuma Timotheo kwenu, aliye mwana wangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakaewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama nifundishavyo killa pahali katika killa kanisa.