1 Corinthians 4:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu, hayo yote niliyosema juu ya Apolo na juu yangu, ni kielelezo kwenu: Kutokana na mfano wangu mimi na Apolo nataka mwelewe maana ya msemo huu: “Zingatieni yaliyoandikwa.” Kati yenu pasiwe na mtu yeyote anayejivunia mtu mmoja na kumdharau mwingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi ndugu zangu, mambo haya nimeyafanya kwangu binafsi na Apolo kwa faida yenu, ili mweze kujifunza kutoka kwetu maana ya ule usemi usemao, “Msivuke zaidi ya yale yaliyoandikwa.” Hivyo hamtajivunia mtu fulani na kumdharau mwingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndugu zangu, nimemtumia Apolo na mimi mwenyewe kama mfano kwa ajili yenu. Nimefanya hivi ili mjifunze kutoka kwetu maana ya maneno yanayosema, “Uwe mwangalifu kufuata kilichoandikwa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu, hayo yote niliyosema juu ya Apolo na juu yangu, ni kielelezo kwenu: kutokana na mfano wangu mimi na Apolo nataka mwelewe maana ya msemo huu: “Zingatieni yaliyoandikwa.” Kati yenu pasiwe na mtu yeyote anayejivunia mtu mmoja na kumdharau mwingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu, hayo yote niliyosema juu ya Apolo na juu yangu, ni kielelezo kwenu: kutokana na mfano wangu mimi na Apolo nataka mwelewe maana ya msemo huu: “Zingatieni yaliyoandikwa.” Kati yenu pasiwe na mtu yeyote anayejivunia mtu mmoja na kumdharau mwingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi ndugu zangu, mambo haya nimeyafanya kuwa mfano wa mimi binafsi na Apolo kwa faida yenu, ili mweze kujifunza kutoka kwetu maana ya ule usemi usemao, “Msivuke zaidi ya yale yaliyoandikwa.” Hivyo hamtajivunia mtu fulani na kumdharau mwingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi ndugu zangu, mambo haya nimeyafanya kwangu binafsi na Apolo kwa faida yenu, ili mweze kujifunza kutoka kwetu maana ya ule usemi usemao, “Msivuke zaidi ya yale yaliyoandikwa.” Hivyo hamtajivunia mtu fulani na kumdharau mwingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu, hayo yote niliyosema juu ya Apolo na juu yangu, ni kielelezo kwenu: Kutokana na mfano wangu mimi na Apolo nataka mwelewe maana ya msemo huu: “Zingatieni yaliyoandikwa.” Kati yenu pasiwe na mtu yeyote anayejivunia mtu mmoja na kumdharau mwingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu, kwa ajili yenu nimeyasema haya kama mfano wa mimi na Apolo, mpate kujifundishia kwetu sisi, msijikweze kupapita hapo palipoandikwa kwamba: Mtu asijitutumue kuwa mkuu kuliko mwenziwe na kumpunguza mwingine!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu zangu, nimesema maneno haya nikitwaa mufano wa Apolo na wangu mimi mwenyewe kusudi yakuwe fundisho kwenu. Nilitaka kwamba kufuatana na mufano huu mujifunze maana ya masemi haya: “Musipite pembeni ya maandiko.” Hata mutu mumoja kati yenu asijivunie mutu fulani na kuzarau mwingine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mambo haya, ndugu, nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na wa Apollo kwa ajili yemi, illi kwa khabari zetu mpate kujifunza katika fikara zenu kutokuruka mpaka wa yale yaliyoandikwa; mtu mmoja asijivune juu ya mwenziwe, kwa ajili ya mtu mwingine.