1 Corinthians 4:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana ni nani aliyewafanya kuwa tofauti na wengine? Ni nini mlicho nacho ambacho hamkupokea? Nanyi kama mlipokea, kwa nini mnajivuna kama vile hamkupokea?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa nini mnajisifu? Mlipewa kila kitu mlicho nacho. Sasa, ikiwa mlipewa kila kitu mlicho nacho, kwa nini mnajisifu kana kwamba mlipata vitu vyote kwa nguvu zenu wenyewe?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ni nani aliyekufanya wewe kuwa tofauti na mwingine? Ni nini ulicho nacho ambacho hukupokea? Nawe kama ulipokea, kwa nini unajivuna kama vile hukupokea?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana ni nani aliyewafanya kuwa tofauti na wengine? Ni nini mlicho nacho ambacho hamkupokea? Nanyi kama mlipokea, kwa nini mnajivuna kama vile hamkupokea?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Yuko anayekupatia wewe macheo zaidi? Unacho kitu gani, usichopewa? Lakini kama umepewa, wajivuniaje, kama hukupewa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni nani aliyekuweka kuwa mukubwa kuliko wengine? Si Mungu ndiye aliyekupa vitu vyote unavyokuwa navyo? Ikiwa ni hivi, kwa sababu gani unajivuna kama vile haukuvipewa kama zawadi?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana ni nani anaekupambanua na mwingine? na una, nini usiyoipokea? Na iwapo uliipokea, wajisifiani kana kwamba hukuipokea?