1 Corinthians 5:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukweli ni kwamba sikuwa na maana ya watu wote duniani walio wazinzi, wachoyo, walaghai na wenye kuabudu sanamu. Maana, ili kuwaepa hao wote ingewalazimu nyinyi kuihama dunia hii kabisa!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sina maana kwamba msishirikiane na wazinzi wa ulimwengu huu, au wenye tamaa mbaya, wanyang’anyi au waabudu sanamu. Kwa kufanya hivyo ingewalazimu mtoke ulimwenguni humu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini sikuwa na maana ya watu wa ulimwengu huu. La sivyo ingewalazimu kuhama katika ulimwengu huu ili mweze kujitenga na wazinzi au walio walafi na waongo, au wale wanaoabudu sanamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ukweli ni kwamba sikuwa na maana ya watu wote duniani walio wazinzi, wachoyo, walaghai na wenye kuabudu sanamu. Maana, ili kuwaepa hao wote ingewalazimu ninyi kuihama dunia hii kabisa!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukweli ni kwamba sikuwa na maana ya watu wote duniani walio wazinzi, wachoyo, walaghai na wenye kuabudu sanamu. Maana, ili kuwaepa hao wote ingewalazimu nyinyi kuihama dunia hii kabisa!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sina maana kwamba msishirikiane na wazinzi wa ulimwengu huu, au wenye tamaa mbaya, wanyang'anyi au waabudu sanamu. Kwa kufanya hivyo ingewalazimu mtoke humu ulimwenguni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sina maana kwamba msishirikiane na wazinzi wa ulimwengu huu, au wenye tamaa mbaya, wanyang’anyi au waabudu sanamu. Kwa kufanya hivyo ingewalazimu mtoke ulimwenguni humu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ukweli ni kwamba sikuwa na maana ya watu wote duniani walio wazinzi, wachoyo, walaghai na wenye kuabudu sanamu. Maana, ili kuwaepa hao wote ingewalazimu nyinyi kuihama dunia hii kabisa!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo sikuwasema wagoni wa ulimwengu huu au wenye choyo na wanyang'anyi au wenye kutambikia mizimu. Kama vingekuwa hivyo, ingewapasa kutoka ulimwenguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hiyo sikusema kabisa kwamba musishirikiane na wote wanaokuwa wazinzi katika dunia hii, wala wenye tamaa, wala wanyanganyi, wala wenye kuabudu sanamu. Kwa maana kwa kujitenga nao, ingewapasa kutoka katika dunia!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sisemi msichangamane kabisa kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani an wanyangʼanyi, an wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.