1 Corinthians 5:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilichoandika ni hiki: Msishirikiane na ndugu Mkristo aliye mzinzi, mchoyo, mwenye kuabudu sanamu, mchongezi, mlevi na mlaghai. Mtu wa namna hiyo, hata kula msile naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa nawaandikia kwamba msishirikiane na mtu yeyote anayejiita ndugu, hali akiwa ni mzinzi, au mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu au msingiziaji, mlevi au mdhalimu. Mtu kama huyo hata msile naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilikuwa na maana kuwa msishirikiane na mtu yeyote yule anayedai kuwa anaamini lakini anaendelea kuishi katika dhambi. Usimkaribishe nyumbani kwa chakula kaka ama dada aliye mzinzi, mlafi, anayeabudu sanamu, mtukanaji, mlevi au mwongo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nilichoandika ni hiki: msishirikiane na ndugu Mkristo aliye mzinzi, mchoyo, mwenye kuabudu sanamu, mchongezi mlevi na mlaghai. Mtu wa namna hiyo, hata kula msile naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilichoandika ni hiki: msishirikiane na ndugu Mkristo aliye mzinzi, mchoyo, mwenye kuabudu sanamu, mchongezi, mlevi na mlaghai. Mtu wa namna hiyo, hata kula msile naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa nawaandikia kwamba msishirikiane na mtu ye yote anayejiita ndugu, hali akiwa ni mzinzi, au mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu au msingiziaji, mlevi au mdhalimu. Mtu kama huyo hata msile naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa nawaandikia kwamba msishirikiane na mtu yeyote anayejiita ndugu, hali akiwa ni mzinzi, au mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu au msingiziaji, mlevi au mdhalimu. Mtu kama huyo hata msile naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, mambo yalivyo, niliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilichoandika ni hiki: Msishirikiane na ndugu Mkristo aliye mzinzi, mchoyo, mwenye kuabudu sanamu, mchongezi, mlevi na mlaghai. Mtu wa namna hiyo, hata kula msile naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hapo nimewaandikia, msichanganyike na mtu aitwaye ndugu, akiwa mgoni au mwenye choyo au mtambikia mizimu au mwenye matusi au mlevi au mnyang'anyi; basi, ndugu aliye hivyo msile naye!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini niliwaandikia kwamba musishirikiane na mutu anayejiita ndugu mwamini, akiwa mwasherati, mwenye tamaa, mwenye kuabudu sanamu, mutukanaji, mulevi au munyanganyi. Na zaidi ya ile musichangie chakula na mutu wa namna hii.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini sasa nimewaandikieni kwamba msichangamane na mtu aitwae ndugu, akiwa mzinzi au mwenye kutamani an mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnangʼanyi; mtu wa namna hii msikubali hatta kula nae.