1 Corinthians 5:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, ni shauri langu kuwahukumu watu walio nje? Hao Mungu atawahukumu. Je, nyinyi hampaswi kuwahukumu wale walio katika jamii yenu nyinyi wenyewe?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yanihusu nini kuwahukumu wale watu walio nje ya kundi la waumini? Je, si mnapaswa kuwahukumu hao walio ndani?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Si kazi yangu kuwahukumu wasio sehemu ya kundi la waamini. Mungu atawahukumu, lakini ni lazima mwahukumu wale walio katika kundi lenu. Maandiko yanasema, “Mwondoe mwovu katika kundi lako.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, ni shauri langu kuwahukumu watu walio nje? Hao Mungu atawahukumu. Je, ninyi hampaswi kuwahukumu wale walio katika jamii yenu ninyi wenyewe?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, ni shauri langu kuwahukumu watu walio nje? Hao Mungu atawahukumu. Je, nyinyi hampaswi kuwahukumu wale walio katika jamii yenu nyinyi wenyewe?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yanihusu nini kuwahukumu wale watu walio nje ya kanisa? Je, si mnapaswa kuwahukumu hao walio ndani ya kanisa?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yanihusu nini kuwahukumu wale watu walio nje ya kundi la waumini? Je, si mnapaswa kuwahukumu hao walio ndani?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamuwahukumu hao walio ndani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, ni shauri langu kuwahukumu watu walio nje? Hao Mungu atawahukumu. Je, nyinyi hampaswi kuwahukumu wale walio katika jamii yenu nyinyi wenyewe?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nina jambo gani nao walioko nje, niwaumbue? Nanyi si kazi yenu kuwaumbua hao, mlionao?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi si kazi yangu kuhukumu wale wanaokuwa wa inje ya kanisa. Mungu ndiye atakayewahukumu. Lakini ninyi hamupaswi kuhukumu watu wa kanisa lenu? Kama vile Maandiko Matakatifu yanavyosema: “Mumwondoe mutu yule mubaya toka katikati yenu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana yanikhusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu walio ndani?