1 Corinthians 6:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Anathubutuje mmoja wenu kumshtaki ndugu mwaamini mbele ya mahakama ya watu wasiomjua Mungu badala ya kumshtaki mbele ya watu wa Mungu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mtu yeyote wa kwenu ana ugomvi na mwenzake, anathubutuje kuupeleka kwa wasiomcha Mungu ili kuamuliwa badala ya kuupeleka kwa watakatifu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa nini mnakwenda kwenye mahakama za kisheria mmoja wenu anapokuwa na shauri dhidi ya mwingine aliye miongoni mwenu? Mnajua ya kwamba mahakimu wa aina hiyo hawawezi kutegemewa kuamua kwa haki iliyo ya kweli. Sasa kwa nini mnawaruhusu wawaamulie aliye na haki? Kwa nini msiwaruhusu watakatifu wa Mungu waamue ni nani aliye na haki?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Anathubutuje mmoja wenu kumshtaki ndugu muumini mbele ya mahakama ya watu wasiomjua Mungu badala ya kumshtaki mbele ya watu wa Mungu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Anathubutuje mmoja wenu kumshtaki ndugu mwaamini mbele ya mahakama ya watu wasiomjua Mungu badala ya kumshtaki mbele ya watu wa Mungu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mtu ye yote wa kwenu ana ugomvi na mwenzake, anathubutuje kuupeleka kwa wasiomcha Mungu ili kuamuliwa badala ya kuupeleka kwa watakatifu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mtu yeyote wa kwenu ana ugomvi na mwenzake, anathubutuje kuupeleka kwa wasiomcha Mungu ili kuamuliwa badala ya kuupeleka kwa watakatifu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Mmoja wenu akiwa ana shitaka juu ya mwenzake athubutuje kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Anathubutuje mmoja wenu kumshtaki ndugu mwaamini mbele ya mahakama ya watu wasiomjua Mungu badala ya kumshtaki mbele ya watu wa Mungu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Inakuwaje, mtu wa kwenu aliye na jambo na mwenziwe akijipa moyo wa kuja kushtaki mbele yao walio wapotovu, asije mbele yao walio watakatifu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati mutu mumoja kati yenu anapokuwa na ugomvi na ndugu mwenzake mwamini, atasubutu namna gani kwenda kumushitaki mbele ya waamuzi wapagani pahali pa kumushitaki mbele ya watu wa Mungu?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
JE! mtu wa kwenu akiwa na neno juu ya mwenzake athubutu kuhukumiwa mbele ya wasio haki wala si mbele ya watakatifu?