1 Corinthians 6:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, ambaye mlimpokea kutoka kwa Mungu? Nyinyi basi, si mali yenu wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu wa Mungu akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nina uhakika mnajua kuwa mwili wenu ni hekalu kwa ajili ya Roho Mtakatifu mliyepewa na Mungu na Roho Mtakatifu anaishi ndani yenu. Hamjimiliki ninyi wenyewe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, ambaye mlimpokea kutoka kwa Mungu? Ninyi basi, si mali yenu wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, ambaye mlimpokea kutoka kwa Mungu? Nyinyi basi, si mali yenu wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni hekalu la Roho wa Mwenyezi Mungu akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mwenyezi Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, ambaye mlimpokea kutoka kwa Mungu? Nyinyi basi, si mali yenu wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au hamjui, ya kuwa miili yenu ni nyumba yake Roho Mtakatifu awakaliaye? Ndiye, mliyepewa na Mungu, ninyi ham wenye ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hamujui kwamba mwili wenu ni hekalu la Roho Mutakatifu anayekuwa ndani yenu, yule muliyepewa na Mungu? Na ninyi si mali yenu wenyewe.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu ya Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyopewa na Mungu? Na ninyi si mali yenu wenyewe;