1 Corinthians 6:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aibu kwenu! Ndiyo kusema hakuna hata mmoja miongoni mwenu mwenye hekima kiasi cha kuweza kutatua tatizo kati ya ndugu waumini?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nasema hivi ili mwone aibu. Je, inawezekana kuwa miongoni mwenu hakuna mtu mwenye hekima ya kutosha kuamua ugomvi kati ya waumini?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninasema hivi ili kuwatahayarisha. Nina uhakika yupo mwenye hekima miongoni mwa waamini katika kanisa lenu anayeweza kutatua mgogoro kati ya waamini wawili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Aibu kwenu! Ndiyo kusema hakuna hata mmoja miongoni mwenu mwenye hekima kiasi cha kuweza kutatua tatizo kati ya ndugu waumini?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aibu kwenu! Ndiyo kusema hakuna hata mmoja miongoni mwenu mwenye hekima kiasi cha kuweza kutatua tatizo kati ya ndugu waumini?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nasema hivi ili mwone aibu. Je, inawezekana kuwa miongoni mwenu hakuna mtu mwenye hekima ya kutosha kuamua ugomvi kati ya ndugu mmoja na mwenzake?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nasema hivi ili mwone aibu. Je, inawezekana kuwa miongoni mwenu hakuna mtu mwenye hekima ya kutosha kuamua ugomvi kati ya waaminio?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aibu kwenu! Ndiyo kusema hakuna hata mmoja miongoni mwenu mwenye hekima kiasi cha kuweza kutatua tatizo kati ya ndugu waumini?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya nayasemea kuwatia soni. Je? Kwenu hakuna hata mmoja mwenye werevu wa kweli awezaye kuamua ndugu na mwenzake?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninasema hivi kwa kuwapatisha haya. Hakika kati yenu hakuna hata mutu mumoja mwenye hekima anayeweza kukata maneno kati ya wandugu zake waamini?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nasema haya nipate kuwatahayarisheni. Je! ndivyo hivyo, kwamba kwenu hakuna hatta mtu mmoja mwenye hekima, awezae kukata maneno ya ndugu zake?