1 Corinthians 7:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
lakini kama akiachana naye, basi abaki bila kuolewa; ama la, apatanishwe na mume wake. Mume naye asimpe talaka mkewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini akitengana, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Wala mume asimpe mkewe talaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ikiwa mke anaondoka, anapaswa kukaa bila kuolewa au arudi kwa mume wake. Na mume hapaswi kumtaliki mke wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
lakini kama akiachana naye, basi abaki bila kuolewa; ama la, apatanishwe na mume wake. Mume naye asimpe talaka mkewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
lakini kama akiachana naye, basi abaki bila kuolewa; ama la, apatanishwe na mume wake. Mume naye asimpe talaka mkewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama akimwacha, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Wala mume asimpe mkewe talaka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini akitengana, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Wala mume asimpe mkewe talaka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
lakini kama akiachana naye, basi abaki bila kuolewa; ama la, apatanishwe na mume wake. Mume naye asimpe talaka mkewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mke akiwa ameachana na mumewe, sharti akae pasipo kuolewa au apatanishwe tena na mumewe! Naye mume asiachane na mkewe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama muke akiachana na mume wake, asiolewe tena, kama si vile apatane tena na mume wake. Vilevile mume hapaswi kufukuza muke wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
lakini, ikiwa ameachana nae, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.