1 Corinthians 7:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa wale wengine, (mimi binafsi, si Bwana) nasema hivi: Ikiwa mwanamume Mkristo anaye mke asiyeamini, na huyo mwanamke akakubali kuendelea kuishi naye, asimpe talaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kwa wengine nasema (si Bwana Isa, ila ni mimi): Kama ndugu ana mke asiyeamini, naye huyo mke anakubali kuishi pamoja naye, basi asimwache.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ushauri nilionao kwa wengine unatoka kwangu. Bwana hajatupa mafundisho mengine kuhusu hili. Ukiwa na mke asiyeamini, usimtaliki ikiwa yuko radhi kuendelea kuishi pamoja nawe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa wale wengine, (mimi binafsi, si Bwana) nasema hivi: Ikiwa mwanamume Mkristo anaye mke asiyeamini, na huyo mwanamke akakubali kuendelea kuishi naye, asimpe talaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa wale wengine, (mimi binafsi, si Bwana) nasema hivi: Ikiwa mwanamume Mkristo anaye mke asiyeamini, na huyo mwanamke akakubali kuendelea kuishi naye, asimpe talaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kwa wengine nasema (si Bwana ila ni mimi): Kama ndugu ana mke asiyeamini, naye huyo mke anakubali kuishi pamoja naye, basi asimwache.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kwa wengine nasema (si Bwana Isa, ila ni mimi): Kama ndugu ana mke asiyeamini, naye huyo mke anakubali kuishi pamoja naye, basi asimwache.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa wale wengine, (mimi binafsi, si Bwana) nasema hivi: Ikiwa mwanamume Mkristo anaye mke asiyeamini, na huyo mwanamke akakubali kuendelea kuishi naye, asimpe talaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wengine nawaambia mimi, si Bwana: Aliye ndugu akiwa na mke asiyemtegemea Mungu, naye mkewe anapenda kukaa naye, asimwache!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa wengine, mimi ninawaambia maneno haya, lakini hayatoki kwa Bwana: kama mume mwamini akiwa na muke asiyeamini, naye muke yule akikubali kuishi pamoja naye, asimufukuze.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana; ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke buyo anakubali kukaa nae, asimwache.