1 Corinthians 7:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama mtu aliitwa akiwa ametahiriwa, basi asijisingizie kwamba hakutahiriwa; na kama alipoitwa hakuwa ametahiriwa, basi na asitahiriwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, mtu alikuwa tayari ametahiriwa alipoitwa? Asijifanye asiyetahiriwa. Je, mtu alikuwa hajatahiriwa alipoitwa? Asitahiriwe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Mtu fulani ameitwa hali amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa hali hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwanaume asibadili tohara yake ikiwa alikuwa ametahiriwa alipoitwa. Ikiwa hakuwa ametahiriwa alipoitwa, asitahiriwe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama mtu aliitwa akiwa ametahiriwa, basi asijisingizie kwamba hakutahiriwa; na kama alipoitwa hakuwa ametahiriwa, basi na asitahiriwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama mtu aliitwa akiwa ametahiriwa, basi asijisingizie kwamba hakutahiriwa; na kama alipoitwa hakuwa ametahiriwa, basi na asitahiriwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, mtu alikuwa ametahiriwa alipoitwa? Asijifanye asiyetahiriwa. Je, mtu alikuwa hajatahiriwa alipoitwa? Asitahiriwe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, mtu alikuwa tayari ametahiriwa alipoitwa? Asijifanye asiyetahiriwa. Je, mtu alikuwa hajatahiriwa alipoitwa? Asitahiriwe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Mtu fulani ameitwa akiwa amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa akiwa hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama mtu aliitwa akiwa ametahiriwa, basi asijisingizie kwamba hakutahiriwa; na kama alipoitwa hakuwa ametahiriwa, basi na asitahiriwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akiitwa alipokwisha kutahiriwa asivifiche! Mtu akiitwa akiwa hajatahiriwa, asitahiriwe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Mtu fulani ameitwa hali amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa hali hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa mutu alitahiriwa mbele ya kuitwa na Mungu, asitafute kufuta kovu la kutahiriwa kwake. Ikiwa alikuwa hajatahiriwa wakati alipoitwa na Mungu, hapaswi kutahiriwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu fullani ameitwa nae amekwisha kutahiriwa? asijifanye kana kwamba hakutabiriwa. Mtu fullani amekwitwa nae hajatahiriwa bado? bassi asitahiriwe.