1 Corinthians 7:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, kuhusu mabikira na waseja, sina amri kutoka kwa Bwana; lakini natoa maoni yangu mimi ambaye kwa huruma yake Bwana nastahili kuaminiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi, kuhusu wale walio bikira, mimi sina amri kutoka kwa Bwana Isa, lakini mimi natoa shauri kama mtu ambaye ni mwaminifu kwa rehema za Bwana Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa nitaandika kuhusu suala jingine mliloniandikia mkiuliza kuhusu watu ambao hawajaoa au kuolewa. Sina amri kutoka kwa Bwana kuhusu hili, lakini haya ni maoni yangu. Na ninaweza kuaminiwa kwa sababu Bwana amenipa rehema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sasa, kuhusu mabikira na waseja, sina amri kutoka kwa Bwana; lakini natoa maoni yangu mimi ambaye kwa huruma yake Bwana nastahili kuaminiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, kuhusu mabikira na waseja, sina amri kutoka kwa Bwana; lakini natoa maoni yangu mimi ambaye kwa huruma yake Bwana nastahili kuaminiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi, kuhusu wale walio bikira, mimi sina amri kutoka kwa Bwana, lakini mimi natoa shauri kama mtu ambaye ni mwaminifu kwa rehema za Bwana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi, kuhusu wale walio bikira, mimi sina amri kutoka kwa Bwana Isa, lakini mimi natoa shauri kama mtu ambaye ni mwaminifu kwa rehema za Bwana Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuhusu wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, kuhusu mabikira na waseja, sina amri kutoka kwa Bwana; lakini natoa maoni yangu mimi ambaye kwa huruma yake Bwana nastahili kuaminiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa ajili ya wanawali sikupata agizo la Bwana, ninawaambia, ninayoyatambua kwa hivyo, nilivyogawiwa na Bwana kuwa mwelekevu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuelekea wale ambao hawajaoa wala kuolewa, sina neno la kuwaamuru kutoka kwa Bwana. Lakini nitawatolea shauri kufuatana na vile ninavyokuwa mutu anayestahili kuaminiwa, kutokana na neema niliyopewa na Bwana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa khabari za mabikira sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kuwa mwaminifu kwa rehema za Bwana.