1 Corinthians 7:28 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ikiwa utaoa hutakuwa umetenda dhambi; na msichana akiolewa hatakuwa ametenda dhambi. Hao watakaooana watapatwa na matatizo ya dunia hii, lakini mimi ningependa hayo yasiwapate nyinyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama ukioa, hujatenda dhambi; na kama bikira akiolewa, hajatenda dhambi. Lakini wale wanaooa watakabiliana na matatizo mengi katika maisha haya, nami nataka kuwazuilia hayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini si dhambi ukiamua kuoa. Lakini waliooa watapata dhiki katika maisha haya, nami ninataka msiipitie dhiki hiyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini ikiwa utaoa hutakuwa umetenda dhambi; na msichana akiolewa hatakuwa ametenda dhambi. Hao watakaooana watapatwa na matatizo ya dunia hii, lakini mimi ningependa hayo yasiwapate ninyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini ikiwa utaoa hutakuwa umetenda dhambi; na msichana akiolewa hatakuwa ametenda dhambi. Hao watakaooana watapatwa na matatizo ya dunia hii, lakini mimi ningependa hayo yasiwapate nyinyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama ukioa, hujatenda dhambi; na kama bikira akiolewa, hajatenda dhambi. Lakini wale wanaooa watakabiliana na matatizo mengi katika maisha haya, nami nataka kuwazuilia hayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama ukioa, hujatenda dhambi; na kama bikira akiolewa, hajatenda dhambi. Lakini wale wanaooa watakabiliana na matatizo mengi katika maisha haya, nami nataka kuwazuilia hayo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ikiwa utaoa hutakuwa umetenda dhambi; na msichana akiolewa hatakuwa ametenda dhambi. Hao watakaooana watapatwa na matatizo ya dunia hii, lakini mimi ningependa hayo yasiwapate nyinyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hata ukioa hukosi, naye mwanamwali akiolewa hakosi. Lakini wafanyao hivyo huipatia miili maumivu, nayo ndiyo, mimi ninayoyataka kuwaponya
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama ukioa, haufanyi zambi, na kama binti anaolewa, yeye hafanyi zambi vilevile. Lakini wale wanaooana watakuwa na mateso katika maisha yao, na mimi ninataka kuwaonya kusudi muepuke mateso yale.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini, kama ukioa, huna khatiya, na bikira akiolewa, hana khatiya; lakini watu hao watakuwa na mateso katika mwili; lakini nataka kuwazuilia haya.