1 Corinthians 7:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
naye amegawanyika. Mwanamke asiyeolewa au bikira hujishughulisha na mambo ya Bwana apate kujitolea mwili na roho kwa Bwana. Lakini mwanamke aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii jinsi atakavyompendeza mumewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na mawazo yake yamegawanyika. Mwanamke asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana: lengo lake ni awe mtakatifu kimwili na kiroho. Lakini yule aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia, jinsi atakavyoweza kumfurahisha mumewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni lazima afikirie mambo mawili; kumpendeza mke wake na kumpendeza Bwana. Mwanamke ambaye hajaolewa au msichana ambaye hajawahi kuolewa hujishughulisha na kazi ya Bwana. Hutaka kuutoa mwili na roho yake kikamilifu kwa Bwana. Lakini mwanamke aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya ulimwengu ili ampendeze mume wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
naye amegawanyika. Mwanamke asiyeolewa au bikira hujishughulisha na mambo ya Bwana apate kujitolea mwili na roho kwa Bwana. Lakini mwanamke aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii jinsi atakavyompendeza mumewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
naye amegawanyika. Mwanamke asiyeolewa au bikira hujishughulisha na mambo ya Bwana apate kujitolea mwili na roho kwa Bwana. Lakini mwanamke aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii jinsi atakavyompendeza mumewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pia kuna tofauti kati ya mwanamke aliyeolewa na msichana bikira. Mwanamke asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana ili awe mtakatifu kimwili na kiroho, lakini yule aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia, jinsi atakavyoweza kumfurahisha mumewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na mawazo yake yamegawanyika. Mwanamke asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana Isa: lengo lake ni awe mtakatifu kimwili na kiroho. Lakini yule aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia, jinsi atakavyoweza kumfurahisha mumewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
naye amegawanyika. Mwanamke asiyeolewa au bikira hujishughulisha na mambo ya Bwana apate kujitolea mwili na roho kwa Bwana. Lakini mwanamke aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii jinsi atakavyompendeza mumewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo ya mke na ya mwanamwali ni yaleyale: mke asiye na mume naye mwanamwali huyasumbukia mambo ya Bwana, apate kutakata mwilini na rohoni. Lakini mwenye mume huyasumbukia mambo ya ulimwenguni, apate kumpendeza mumewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye anashugulikia mambo mawili. Vilevile mwanamuke asiyeolewa au binti anashugulikia mambo ya Bwana. Anajitolea kwa Bwana katika mawazo na matendo yake yote. Lakini mwanamuke anayeolewa, anashugulikia mambo ya dunia, anatafuta jinsi ya kumupendeza mume wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena iko tofauti hii kati ya mke na hikira. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu katika mwili na katika roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia, jinsi atakavyompendeza mumewe.