1 Corinthians 7:35 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawaambieni haya kwa faida yenu, na si kwa kuwawekeeni kizuizi. Nataka tu muwe na mpango unaofaa, mpate kumtumikia Bwana kwa moyo na nia moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninasema haya kwa faida yenu wenyewe, sio ili kuwawekea vizuizi bali mpate kuishi kwa jinsi ilivyo vyema bila kuvutwa pengine katika kujitoa kwenu kwa Bwana Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninasema hili ili niwasaidie. Si kuwawekea vikwazo, lakini ninataka mwishi katika njia sahihi. Na ninataka mjitoe kikamilifu kwa Bwana pasipo kuchukuliwa katika mambo mengine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nawaambieni haya kwa faida yenu, na si kwa kuwawekeeni kizuio. Nataka tu muwe na mpango unaofaa, mpate kumtumikia Bwana kwa moyo na nia moja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawaambieni haya kwa faida yenu, na si kwa kuwawekeeni kizuizi. Nataka tu muwe na mpango unaofaa, mpate kumtumikia Bwana kwa moyo na nia moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninasema haya kwa faida yenu, sio ili kuwawekea kizuizi cho chote, bali mpate kuishi kwa jinsi ilivyo vyema bila kuvutwa pengine katika kujitoa kwenu kwa Bwana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninasema haya kwa faida yenu wenyewe, sio ili kuwawekea vizuizi bali mpate kuishi kwa jinsi ilivyo vyema bila kuvutwa pengine katika kujitoa kwenu kwa Bwana Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawaambieni haya kwa faida yenu, na si kwa kuwawekeeni kizuizi. Nataka tu muwe na mpango unaofaa, mpate kumtumikia Bwana kwa moyo na nia moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini haya nayasema, kwa kuwa yanawafaa; siyasemi, niwategee kitanzi, ila nayasemea kwamba: Yenu yote yaendelee, kama yapasavyo, mfulize kumkalia Bwana pasipo kuzuiliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maneno hayo ninayosema ni kwa faida yenu, wala si kwa kuwafungia njia. Ninataka kuwaonyesha namna ya kuishi sawa inavyofaa, kusudi mupate kumutumikia Bwana pasipo kizuizo chochote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nasema haya niwafaidie; si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, na mpate kumkhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.