1 Corinthians 7:39 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwanamke aliyeolewa huwa amefungwa na mumewe kwa muda wote mumewe aishipo. Lakini mumewe akifa, mama huyo yuko huru, na akipenda anaweza kuolewa na mtu yeyote, mradi tu iwe Kikristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwanamke aliyeolewa amefungwa na sheria maadamu mumewe yu hai. Lakini mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, lakini lazima awe katika Bwana Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwanamke anapaswa kuishi na mume wake kipindi chote mumewe anapokuwa hai. Lakini mume akifa, mwanamke anakuwa huru kuolewa na mwanaume yeyote. Lakini mwanaume huyo lazima awe yule wa Bwana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwanamke huwa amefungwa na mumewe kwa muda wote mumewe aishipo. Lakini mumewe akifa, mama huyo yuko huru, na akipenda anaweza kuolewa na mtu yeyote, mradi tu iwe Kikristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwanamke aliyeolewa huwa amefungwa na mumewe kwa muda wote mumewe aishipo. Lakini mumewe akifa, mama huyo yuko huru, na akipenda anaweza kuolewa na mtu yeyote, mradi tu iwe Kikristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwanamke aliyeolewa amefungwa na sheria maadamu mumewe yu hai. Lakini kama mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, lakini lazima tu awe katika Bwana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwanamke aliyeolewa amefungwa na sheria maadamu mumewe yu hai. Lakini mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, lakini lazima awe katika Bwana Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yuko hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yuko huru kuolewa na mtu yeyote amtakaye; katika Bwana tu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwanamke aliyeolewa huwa amefungwa na mumewe kwa muda wote mumewe aishipo. Lakini mumewe akifa, mama huyo yuko huru, na akipenda anaweza kuolewa na mtu yeyote, mradi tu iwe Kikristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mke yuko na mwiko siku zote za kuishi kwake mumewe; lakini mumewe anapokufa, amefunguliwa kuolewa naye ye yote, ampendaye, ikiwa tu, kama Bwana atakavyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwanamuke aliyeolewa anafungwa na Sheria katika maisha yake na mume wake wakati mume wake angali muzima. Lakini kama mume wake akikufa, yeye ni huru kuolewa na yule anayetaka, lakini sherti ndoa ikuwe ya kikristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwanamke hufungwa maadam mumewe yu hayi, lakini iki va mumewe amefariki, yu huru; aweza kuolewa na mtu ye yote amtakae; katika Bwana tu.