1 Corinthians 7:40 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, nionavyo mimi, atakuwa na heri zaidi kama akibaki hivyo alivyo. Hayo ni maoni yangu, na nafikiri mimi pia ninaye Roho wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kwa maoni yangu, angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo. Nami nadhani pia nina Roho wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini heri yeye zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi, nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho wa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa atabaki kuwa mjane, atakuwa na furaha sana. Haya ni maoni yangu, na ninaamini yanatoka kwa Roho wa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, nionavyo mimi, atakuwa na heri zaidi kama akibaki hivyo alivyo. Hayo ni maoni yangu, na nafikiri mimi pia ninaye Roho wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, nionavyo mimi, atakuwa na heri zaidi kama akibaki hivyo alivyo. Hayo ni maoni yangu, na nafikiri mimi pia ninaye Roho wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kwa uamuzi wangu, naona kuwa angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo. Nami nadhani pia nina Roho wa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kwa maoni yangu, angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo. Nami nadhani pia nina Roho wa Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini heri yeye zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi, nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho wa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, nionavyo mimi, atakuwa na heri zaidi kama akibaki hivyo alivyo. Hayo ni maoni yangu, na nafikiri mimi pia ninaye Roho wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini vitakavyomfaa kupita hivi ni kukaa hivyo, alivyo. Hivyo ndivyo, nionavyo mimi; lakini najiwazia, ya kwamba nami ninayo Roho ya Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini heri yeye zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi, nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho wa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ingekuwa heri zaidi kama angekaa sawa vile anavyokuwa. Hilo ni shauri langu, nami vilevile ninazani kwamba ninaongozwa na Roho wa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini yu kheri zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi; nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho ya Bwana.