1 Corinthians 7:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msinyimane haki zenu, isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa kitambo tu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara, ili Shetani asije akawajaribuni kwa sababu ya udhaifu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda, ili mweze kujitoa kwa maombi. Kisha mrudiane tena, ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Msinyimane miili yenu. Lakini mnaweza kukubaliana kutojamiiana kwa muda ili mtumie muda huo katika maombi. Kisha mkutane tena ili Shetani asiwajaribu kutokana na kushindwa kujizuia tamaa zenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Msinyimane haki zenu, isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa kitambo tu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara, ili Shetani asije akawajaribu kwa sababu ya udhaifu wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msinyimane haki zenu, isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa kitambo tu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara, ili Shetani asije akawajaribuni kwa sababu ya udhaifu wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkarudiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msinyimane haki zenu, isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa kitambo tu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara, ili Shetani asije akawajaribuni kwa sababu ya udhaifu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msinyamane, isipokuwa mmepatana kukaa hivyo kitambo kidogo, mjipatie siku za kufunga na za kuomba. Kisha mwandamane tena, Satani asipate kuwajaribu, kwani hamwezi kuvumilia pasipo kukoma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musinyimane, isipokuwa tu mumepatana na kwa muda tu kusudi mupate wakati wa kujitoa kwa kufunga na kuomba. Kisha munaweza kurudiliana tena kusudi Shetani asiwajaribu katika uzaifu wenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, illi mpate faragha kwa kufunga na kuomba, mkajiane tena, Shetani asije akawajarihu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.