1 Corinthians 7:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wale ambao hawajaoa na wale walio wajane nawaambia kwamba ni vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa wale wasiooa na kwa wajane, nasema hivi, ingekuwa vizuri wasioe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa kwa ajili ya wale ambao hawajaoa ama hawajaolewa na kwa ajili ya wajane ninawaambia ya kwamba ni vizuri mkae bila kuoa au kuolewa kama mimi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wale ambao hawajaoana na wale walio wajane nawaambia kwamba ni vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wale ambao hawajaoa na wale walio wajane nawaambia kwamba ni vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa wale wasiooa na kwa wajane, ingekuwa vizuri wabaki kama mimi nilivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa wale wasiooa na kwa wajane, nasema hivi, ingekuwa vizuri wasioe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wale ambao hawajaoa na wale walio wajane nawaambia kwamba ni vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wasiooa na wajane nawaambia: Itawafalia, wakikaa kama mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa wale wasiooa bado na wajane, ninawaambia kwamba ingekuwa vema waendelee kuishi peke yao kama vile mimi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni kheri wakae kama mimi nilivyo.