1 Corinthians 8:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, si kila mtu anao ujuzi huu. Maana wako watu wengine waliokwisha zoea sanamu, watu ambao mpaka hivi sasa wanapokula vyakula huviona bado kama vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Na kwa vile dhamiri zao ni dhaifu, hutiwa unajisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini si wote wanaojua jambo hili. Baadhi ya watu bado wamezoea sanamu kuwa halisi hivi kwamba wanapokula chakula kama hicho wanadhani kimetolewa sadaka kwa sanamu na kwa kuwa dhamiri zao ni dhaifu, dhamiri yao inanajisika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali ujuzi huu haumo ndani ya watu wote; ila wengine kwa kuizoelea ile sanamu hata sasa hula kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu; na dhamiri zao, kwa kuwa dhaifu, hunajisika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini si watu wote wanaojua hili. Baadhi ya watu walikuwa na tabia ya kuabudu sanamu huko nyuma. Hivyo wanapokula nyama, bado wanahisi kuhukumiwa kana kwamba wanakula nyama iliyotolewa kwa sanamu. Hawana uhakika ikiwa ni sahihi kula nyama.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, si kila mtu anao ujuzi huu. Maana wako watu wengine waliokwisha zoea sanamu, watu ambao mpaka hivi sasa wanapokula vyakula huviona bado kama vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Na kwa vile dhamiri zao ni dhaifu, hutiwa unajisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, si kila mtu anao ujuzi huu. Maana wako watu wengine waliokwisha zoea sanamu, watu ambao mpaka hivi sasa wanapokula vyakula huviona bado kama vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Na kwa vile dhamiri zao ni dhaifu, hutiwa unajisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini si wote wanaojua jambo hili. Baadhi ya watu bado wamezoea kufikiria kuwa sanamu ni halisi hivyo wanapokula chakula kama hicho wanadhani kimetolewa sadaka kwa sanamu na kwa kuwa dhamiri zao ni dhaifu, kinatiwa unajisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini si wote wanaojua jambo hili. Baadhi ya watu bado wamezoea sanamu kuwa halisi hivi kwamba wanapokula chakula kama hicho wanadhani kimetolewa sadaka kwa sanamu na kwa kuwa dhamiri zao ni dhaifu, dhamiri yao inanajisika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali ujuzi huu haumo ndani ya watu wote; ila wengine kwa kuizoelea ile sanamu hata sasa hula kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu; na dhamiri zao, kwa kuwa dhaifu, hunajisika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, si kila mtu anao ujuzi huu. Maana wako watu wengine waliokwisha zoea sanamu, watu ambao mpaka hivi sasa wanapokula vyakula huviona bado kama vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Na kwa vile dhamiri zao ni dhaifu, hutiwa unajisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sio wote walio wenye utambuzi huu. Kwa hivyo, walivyozoea kutambikia mizimu, hata sasa wako wanaozila zile nyama, zikiwa za tambiko, lakini mioyo yao iliyo minyonge huchafuliwa kwa kujua maana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali ujuzi huu haumo ndani ya watu wote; ila wengine kwa kuizoelea ile sanamu hata sasa hula kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu; na dhamiri zao, kwa kuwa dhaifu, hunajisika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini si watu wote wanaofahamu mambo hayo. Wengi wamezoea kutambikia sanamu za miungu mpaka sasa, wanakula nyama wakizihesabu hakika kuwa za kutambikia sanamu zile. Kwa sababu zamiri yao ni mbovu, wanajisikia kwamba wanajichafua kwa kula chakula kile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bali elimu hii haimo ndani ya watu wote; illa wengine kwa kuizoelea ile sanamu hatta sasa hula kama ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu; na dhamiri yao, kwa kuwa dhaifu, hunajisika.