1 Corinthians 8:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, jihadharini: Huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini angalieni jinsi mnavyotumia uhuru wenu usije ukawa kikwazo kwao walio dhaifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini iweni makini na uhuru wenu. Uhuru wa kula kitu unaweza kuwafanya walio na mashaka wakaanguka katika dhambi kwa kula vyakula hivyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, jihadharini: huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, jihadharini: huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini angalieni jinsi mnavyotumia uhuru wenu usije ukawa kikwazo kwao walio dhaifu katika imani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini angalieni jinsi mnavyotumia uhuru wenu usije ukawa kikwazo kwao walio dhaifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, jihadharini: Huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwangalie tu, matumio yenu yasikwaze wanyonge!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, muangalie vizuri kusudi uhuru wenu usiangushe wale wanaokuwa zaifu katika imani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaze wale walio dhaifu.