1 Corinthians 9:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, hamjui kwamba wanaotumikia hekaluni hupata chakula chao hekaluni, na kwamba wanaotoa sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, hamjui kwamba, watu wafanyao kazi hekaluni hupata chakula chao kutoka hekaluni, nao wale wahudumiao madhabahuni hushiriki kile kitolewacho madhabahuni?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakika mnajua ya kuwa wanaotumika Hekaluni hula chakula kutoka Hekaluni. Na wale wanaotumika madhabahuni hupata sehemu ya yale yanayotolewa madhabahuni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, hamjui kwamba wanaotumikia Hekaluni hupata chakula chao Hekaluni, na kwamba wanaotolea sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, hamjui kwamba wanaotumikia hekaluni hupata chakula chao hekaluni, na kwamba wanaotoa sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, hamjui kwamba, watu wafanyao kazi Hekaluni hupata chakula chao kutoka Hekaluni, nao wale wahudumiao madhabahuni hushiriki kile kitolewacho madhabahuni?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, hamjui kwamba, watu wafanyao kazi hekaluni hupata chakula chao kutoka hekaluni, nao wale wahudumiao madhabahuni hushiriki kile kitolewacho madhabahuni?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiayo madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, hamjui kwamba wanaotumikia hekaluni hupata chakula chao hekaluni, na kwamba wanaotoa sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hamjui, ya kuwa hao watumikiao Patakatifu hula yatokayo Patakatifu? Nao wachinja ng'ombe za tambiko hugawiwa fungu lao hapo chinjioni?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munajua hakika kuwa wale wanaotumika katika hekalu wanapata chakula chao ndani ya hekalu. Na wale wanaotumika kwa kutoa sadaka juu ya mazabahu wanapata sehemu yao kutoka sadaka zile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula sehemu ya vitu vya hekalu, na wale waikhudumiao madhbahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhbahu?