1 Corinthians 9:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa ninaihubiri injili, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumu nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri injili!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ninapohubiri Injili siwezi kujisifu maana ninalazimika kuhubiri. Ole wangu nisipoihubiri Injili!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sijivuni kwa sababu ya kazi yangu ya kuhubiri Habari Njema kwa sababu ni wajibu wangu ambao ni lazima nifanye; ole wangu nisipowahubiri watu Habari Njema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ikiwa ninaihubiri Habari Njema, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumu nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri Habari Njema!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa ninaihubiri injili, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumu nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri injili!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ninapohubiri injili siwezi kujisifu maana ninalazimika kuhubiri. Ole wangu nisipoihubiri Injili!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ninapohubiri Injili siwezi kujisifu maana ninalazimika kuhubiri. Ole wangu nisipoihubiri Injili!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikiwa ninaihubiri injili, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumu nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri injili!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nikiipiga hiyo mbiu njema sinalo la kujivunia, maana nitashurutishwa. Kwani nisipoipiga hiyo mbiu njema ningepatwa na mambo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi sina haki ya kujisifu kwa sababu ninatangaza Habari Njema, kwa maana nimelazimishwa kuitangaza. Basi ole kwangu kama nisipotangaza Habari Njema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana, ijapokuwa naikhubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimepewa sharti; tena ole wangu nisipoikhubiri.