1 Corinthians 9:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, ingawa mimi si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu ili nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa mimi ni huru, wala si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu, ili niweze kuwavuta wengi kadiri iwezekanavyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Niko huru. Similikiwi na mtu yeyote, lakini ninakuwa mtumwa ili watu wengi waokoke.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo, ingawa mimi si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu ili nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, ingawa mimi si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu ili nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa mimi ni huru, wala si mtumwa wa mtu ye yote, nimejifanya kuwa mtumwa wa kila mtu, ili niweze kuwavuta wengi zaidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa mimi ni huru, wala si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya kuwa mtumwa wa kila mtu, ili niweze kuwavuta wengi kadri iwezekanavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nilijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, ingawa mimi si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu ili nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana mimi niliyekombolewa katika utumwa wote nimejigeuza kuwa mtumwa wao wote, kusudi walio wengi niwapate, wanifuate.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi si mutumwa wa mutu yeyote. Lakini nimejifanya kuwa mutumwa wa watu kusudi nipate wengi kati yao sawa inavyowezekana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, illi nipate watu wengi zaidi.