1 Corinthians 9:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata kama kwa watu wengine mimi si mtume, lakini walau kwenu nyinyi mimi ni mtume. Nyinyi ni uthibitisho wa utume wangu kwa sababu ya kuungana kwenu na Bwana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata kama mimi si mtume kwa wengine, hakika mimi ni mtume kwenu, kwa maana ninyi ni muhuri wa utume wangu katika Bwana Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, lakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana ninyi ndinyi muhuri ya utume wangu katika Bwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wengine wanaweza wasikubali kuwa mimi ni mtume, lakini hakika ninyi mnakubali. Ninyi ni uthibitisho kuwa mimi ni mtume wa Bwana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata kama kwa watu wengine mimi si mtume, lakini walau kwenu ninyi mimi ni mtume. Ninyi ni uthibitisho wa mtume wangu kwa sababu ya kuungana kwenu na Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata kama kwa watu wengine mimi si mtume, lakini walau kwenu nyinyi mimi ni mtume. Nyinyi ni uthibitisho wa utume wangu kwa sababu ya kuungana kwenu na Bwana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata kama mimi si mtume kwa wengine, hakika mimi ni mtume kwenu, kwa maana ninyi ni chapa ya utume wangu katika Bwana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata kama mimi si mtume kwa wengine, hakika mimi ni mtume kwenu, kwa maana ninyi ni mhuri wa utume wangu katika Bwana Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, lakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana ninyi ndinyi mhuri wa utume wangu katika Bwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata kama kwa watu wengine mimi si mtume, lakini walau kwenu nyinyi mimi ni mtume. Nyinyi ni uthibitisho wa utume wangu kwa sababu ya kuungana kwenu na Bwana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nisipokuwa mtume wa wengine, lakini ninyi ndimi mtume wenu. Kwani ninyi m muhuri inayoujulisha utume wangu, ya kuwa ni wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, lakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana ninyi ndinyi muhuri ya utume wangu katika Bwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata ikiwa watu wengine hawakubali kuwa mimi ni mutume, ninyi munakubali kuwa mimi ni mutume. Ninyi ni kitambulisho kinachohakikisha kwamba mimi ni mutume, kwa ajili ya kuungana kwenu na Bwana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, illakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana muhuri ya utume wangu ni ninyi katika Bwana.