1 Corinthians 9:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na kwa wale walio nje ya sheria, naishi kama wao, nje ya sheria, ili niwapate hao walio nje ya sheria. Hii haimaanishi kwamba mimi niko nje ya sheria ya Mungu, maana nabanwa na sheria ya Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa watu wasio na Torati nilikuwa kama asiye na Torati (ingawa siko huru mbali na Torati ya Mungu, bali niko chini ya sheria ya Al-Masihi), ili niweze kuwapata wale wasio na sheria.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa wasio na sheria nilikuwa kama nisiye na sheria, ili niwasaidie wasio na sheria kuokoka. Mimi si kama mtu asiye na Sheria ya Mungu, ninatawaliwa na sheria ya Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na kwa wale walio nje ya Sheria, naishi kama wao, nje ya Sheria, ili niwapate hao walio nje ya Sheria. Hii haimaanishi kwamba mimi niko nje ya sheria ya Mungu, maana nabanwa na sheria ya Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na kwa wale walio nje ya sheria, naishi kama wao, nje ya sheria, ili niwapate hao walio nje ya sheria. Hii haimaanishi kwamba mimi niko nje ya sheria ya Mungu, maana nabanwa na sheria ya Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa watu wasio na Sheria nilikuwa kama asiye na Sheria (ingawa siko huru mbali na Sheria ya Mungu, bali niko chini ya Sheria ya Kristo), ili niweze kuwapata wale wasio na Sheria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa watu wasio na sheria nilikuwa kama asiye na sheria (ingawa siko huru mbali na Torati ya Mungu, bali niko chini ya sheria ya Al-Masihi), ili niweze kuwapata wale wasio na sheria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa wale wasio na sheria nilikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na kwa wale walio nje ya sheria, naishi kama wao, nje ya sheria, ili niwapate hao walio nje ya sheria. Hii haimaanishi kwamba mimi niko nje ya sheria ya Mungu, maana nabanwa na sheria ya Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwao wasiojua maonyo nimekuwa kama mwenzao asiyejua maonyo, tena sipo pasipo Maonyo yake Mungu, kwani nayakalia Maonyo yake Kristo; huko ni kwamba tu, niwapate nao wasiojua maonyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile ninapokuwa kati ya wasioishi chini ya Sheria ya Musa, ninaishi kama wao, bila kuangalia Sheria, kusudi niwapate. Hii si kusema kwamba mimi sishiki sheria ya Mungu, kwa maana mimi ni chini ya uongozi wa sheria ya Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa wale wasio na sharia nalikuwa kama sina sharia. Si kana kwamba sina sharia mbele za Mungu, hali mwenye sharia mbele za Kristo, illi niwapate wasio na sharia.