1 Corinthians 9:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwao walio dhaifu nimejifanya dhaifu ili niwapate hao walio dhaifu. Nimejifanya kila kitu kwa wote ili nipate kuwaokoa baadhi yao kwa kila njia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa walio dhaifu nilikuwa dhaifu, ili niweze kuwapata walio dhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia yoyote niweze kuwaokoa baadhi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa waliodhaifu, nilikuwa dhaifu ili niwasaidie kuokoka. Nilifanyika kila kitu kwa watu wote ili nifanye kila kinachowezekana niweze kuwasaidia watu waokolewe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwao walio dhaifu nimejifanya dhaifu ili niwapate hao walio dhaifu. Nimejifanya kila kitu kwa wote ili nipate kuwaokoa baadhi yao kwa kila njia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwao walio dhaifu nimejifanya dhaifu ili niwapate hao walio dhaifu. Nimejifanya kila kitu kwa wote ili nipate kuwaokoa baadhi yao kwa kila njia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa walio dhaifu nilikuwa dhaifu, ili niweze kuwapata walio dhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia yo yote niweze kuwaokoa baadhi yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa walio dhaifu nilikuwa dhaifu, ili niweze kuwapata walio dhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia yoyote niweze kuwaokoa baadhi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa wanyonge nilikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwao walio dhaifu nimejifanya dhaifu ili niwapate hao walio dhaifu. Nimejifanya kila kitu kwa wote ili nipate kuwaokoa baadhi yao kwa kila njia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwao walio wanyonge nimekuwa kama mnyonge mwenzao, niwapate walio wanyonge nao. Hivyo wote nimejifananisha nao katika mambo yo yote, nipate po pote wenye kuokoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa wale wanaokuwa zaifu katika imani, ninajifanya kama muzaifu kusudi niwapate hao wanaokuwa zaifu. Kwa wote nimejifunza kuwa mwenye hali kama yao, kusudi nipate kuokoa wamoja kati yao kwa njia mbalimbali.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, illi niwapate wanyonge. Nalikuwa mtu wa hali zote kwa watu wote, illi nipate kuwaokoa watu kwa njia zote.