1 Corinthians 9:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni mmoja tu anayejinyakulia zawadi?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, hamjui kwamba katika mashindano ya mbio wote wanaoshindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu apewaye tuzo? Kwa hiyo kimbieni katika mashindano ili mkapata tuzo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnajua kuwa katika riadha, wanariadha wengi hukimbia, lakini mmoja tu hupata zawadi. Hivyo kimbieni hivyo. Kimbieni ili mshinde!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni mmoja tu anayejinyakulia zawadi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni mmoja tu anayejinyakulia zawadi?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, hamjui kwamba katika mashindano ya mbio wote wanaoshindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu apewaye tuzo? Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa jinsi ambavyo mtapata tuzo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, hamjui kwamba katika mashindano ya mbio wote wanaoshindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu apewaye tuzo? Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa jinsi ambavyo mtapata tuzo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni mmoja tu anayejinyakulia zawadi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Hamjui: Penye mashindano wote hupiga mbio, lakini atakayepewa tunzo ni mmoja tu? Nanyi pigeni mbio hivyo, kusudi mpewe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munajua hakika kuwa wale wanaofanya mashindano ya kukimbia, wote wanakimbia lakini ni mumoja tu anayepokea zawadi. Basi mukimbie hata mufikie kupokea zawadi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hamjui, ya kuwa washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeao tunzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, illi mpate.