1 Corinthians 9:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanariadha hujipa mazoezi na nidhamu kali; hufanya hivyo ili wajipatie taji iharibikayo! Lakini sisi twafanya hivyo tupate taji isiyoharibika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao hufanya hivyo ili wapokee taji lisilodumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata taji linalodumu milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wote wanaoshiriki katika mchezo hufanya mazoezi kwa bidii ili waweze kushinda na kupata zawadi. Lakini zawadi wanazopata hazidumu milele. Lakini zawadi yetu ni ile inayodumu milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wanariadha hujipa mazoezi na nidhamu kali; hufanya hivyo ili wajipatie taji iharibikayo! Lakini sisi twafanya hivyo tupate taji ya kudumu daima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanariadha hujipa mazoezi na nidhamu kali; hufanya hivyo ili wajipatie taji iharibikayo! Lakini sisi twafanya hivyo tupate taji isiyoharibika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao hufanya hivyo ili wapokee taji isiyodumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata taji idumuyo milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao hufanya hivyo ili wapokee taji isiyodumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata taji idumuyo milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo ili wapokee taji liharibikayo; bali sisi tupokee taji lisiloharibika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanariadha hujipa mazoezi na nidhamu kali; hufanya hivyo ili wajipatie taji iharibikayo! Lakini sisi twafanya hivyo tupate taji isiyoharibika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kila aendaye kushindania hujinyima yote; hao hujinyima, wapewe kilemba kiangamiacho, lakini ninyi mjinyime, mpewe kilemba kisichoangamika!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kila mutu anayefanya mashindano katika michezo anajizuiza na vitu vingi katika mazoezi yake. Basi wanafanya hivi kusudi wapate taji yenye kuharibika; lakini sisi tunafanya vile, kusudi tupate taji isiyoharibika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na killa ashindanae hujiweza katika yote: bassi hao kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi isiyoharibika.