1 Corinthians 9:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, mwanajeshi gani anayelipia utumishi wake jeshini? Mkulima gani asiyekula matunda ya shamba lake la mizabibu? Mchungaji gani asiyekunywa maziwa ya mifugo yake?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni askari yupi aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye shamba la mizabibu na asile matunda yake? Ni nani achungaye kundi na asipate maziwa yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni askari gani aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi la kondoo na hanywi maziwa?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, mwanajeshi gani anayelipia utumishi wake jeshini? Mkulima gani asiyekula matunda ya shamba lake la mizabibu? Mchungaji gani asiyekunywa maziwa ya mifugo yake?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, mwanajeshi gani anayelipia utumishi wake jeshini? Mkulima gani asiyekula matunda ya shamba lake la mizabibu? Mchungaji gani asiyekunywa maziwa ya mifugo yake?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni askari yupi aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni mkulima gani apandaye shamba la mizabibu na asile matunda yake? Ni nani achungaye kundi na asipate maziwa yake hata kidogo?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni askari yupi aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye shamba la mizabibu na asile matunda yake? Ni nani achungaye kundi na asipate maziwa yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni askari gani aendaye vitani wakati wowote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, mwanajeshi gani anayelipia utumishi wake jeshini? Mkulima gani asiyekula matunda ya shamba lake la mizabibu? Mchungaji gani asiyekunywa maziwa ya mifugo yake?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yuko askari aendaye vitani na kujilipa mwenyewe? Yuko mpanda mizabibu asiyekula matunda yao? Au yuko mchunga kundi asiyetumia maziwa ya kundi kuwa kitoweo?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni askari gani anayejilipia mwenyewe vifaa vya kiaskari? Au ni muchungaji gani asiyekunywa maziwa ya kundi analochunga?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nani aendae vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Nani apandae mizabibu asiokula baadhi ya matunda yake? Au nani achungae kundi, asiyekula haadhi ya maziwa ya kundi?