1 John 2:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawaandikieni nyinyi watoto kwa sababu mnamjua Baba. Nawaandikieni nyinyi kina baba kwa kuwa mnamjua yeye ambaye amekuwako tangu mwanzo. Nawaandikieni nyinyi vijana kwa sababu mna nguvu; neno la Mungu limo ndani yenu na mumemshinda yule Mwovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nawaandikia ninyi akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninawaandikia ninyi watoto, kwa sababu mnamjua Baba. Ninawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mnamfahamu yeye aliyekuwepo tangu mwanzo. Ninawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu. Mafundisho ya Neno la Mungu yimo ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nawaandikieni ninyi watoto, kwa sababu mnamjua Baba. Nawaandikieni ninyi kina baba, kwa kuwa mnamjua yeye ambaye amekuwako tangu mwanzo. Nawaandikieni ninyi vijana kwa sababu mna nguvu; neno la Mungu limo ndani yenu na mmemshinda yule Mwovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawaandikieni nyinyi watoto kwa sababu mnamjua Baba. Nawaandikieni nyinyi kina baba kwa kuwa mnamjua yeye ambaye amekuwako tangu mwanzo. Nawaandikieni nyinyi vijana kwa sababu mna nguvu; neno la Mungu limo ndani yenu na mumemshinda yule Mwovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nawaandikia ninyi akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nawaandikia ninyi akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawaandikieni nyinyi watoto kwa sababu mnamjua Baba. Nawaandikieni nyinyi kina baba kwa kuwa mnamjua yeye ambaye amekuwako tangu mwanzo. Nawaandikieni nyinyi vijana kwa sababu mna nguvu; neno la Mungu limo ndani yenu na mumemshinda yule Mwovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naliwaandikia ninyi mlio wana, kwani mmemtambua Baba. Naliwaandikia ninyi mlio baba, kwani mmemtambua yeye aliye mwenye kuwapo tangu mwanzo. Naliwaandikia ninyi mlio vijana, kwani mko na nguvu, hata Neno la Mungu linakaa mwenu, nanyi mmemshinda yule Mbaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimewaandikia ninyi watoto, kwa sababu mumemujua Baba. Ninawaandikia ninyi wababa, kwa sababu mumemujua yule aliyekuwa tangia mwanzo wa vitu vyote. Ninawaandikia ninyi vijana, kwa sababu muko na nguvu na Neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mumemushinda yule Mwovu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu m hodari, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu.