1 John 2:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Dunia inapita, na mambo yote ambayo watu wanayataka kutoka katika dunia nayo yanapita. Lakini yeyote atendaye mambo ambayo Mungu anayataka ataishi milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ulimwengu huu utapita pamoja na tamaa zake; lakini ayafanyaye, Mungu ayatakayo, hukaa kale na kale.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Dunia inapita pamoja na tamaa zake, lakini mutu yule anayefanya mapenzi ya Mungu anaishi milele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na dunia inapita, na tamaa yake, bali yeye afanyae mapenzi ya Mungu adumu hatta milele.