1 John 2:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamwujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siwaandikii kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua, nanyi mnajua hakuna uongo unaotoka katika kweli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnadhani ninawaandikia waraka huu kwa sababu hamuijui kweli? Hapana! Ninawaandikia kwa sababu mnaijua kweli. Na mnajua kuwa hakuna uongo utokao katika kweli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamuujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamwujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siwaandikii kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua, nanyi mnajua hakuna uongo utokao katika kweli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siwaandikii kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua, nanyi mnajua hakuna uongo utokao katika kweli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mnaijua, tena kwamba hapana uongo wowote utokao katika hiyo kweli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamwujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sikuwaandikia ninyi, kwa sababu hamkuyajua yaliyo ya kweli, ila kwa sababu mmeyajua, tena mmejua, ya kuwa hakuna uwongo utokao kwenye ukweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, sikuwaandikia kwa sababu hamujui ukweli, lakini kwa sababu munaujua na tena kwa sababu hakuna uongo wowote unaoweza kutokana na ukweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sikuwaandikia ninyi, kwa sababu hamwijui kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uwongo wo wote utokao katika kweli.